Mwamuzi wa Tanga kuamua vita ya watani Kesho
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Hance Mabena kutoka Tanga kuwa mwamuzi wa mchezo wa kesho wa Ligi KuuTanzania Bara kati ya Yanga na Simba utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mabena atakayesimama katikati, atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga pamoja na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam watakaosimama pembeni wakati Elly Sasii kutoka Dar es salaam atakuwa mwamuzi wa akiba.
Viingilio katika mchezo huo VIP A Tsh 30000, B na C Tsh 20000 na mzunguko ni Tsh 7000