Juventus kumnasa Icardi
Baada ya mshambuliaji Mauro Icardi kuvuliwa unahodha wa klabu yake ya Inter Milan kufuatia maneno aliyoyatoa mke wake ambaye pia ni wakala wake Wanda Nara kuwa mumewe na mteja wake anatengwa na wachezaji wenzake kiasi cha kutopewa ushirikiano wa kutosha akafunga, leo zimeripotiwa taarifa na chanzo cha kuaminika kuwa nyota huyo anakwenda Juventus.
Taarifa za Mauro Icardi kuvuliwa unahodha ziliambatana na tetesi kuwa na kocha wake kaamua kumuacha nyota huyo katika safari ya kwenda kucheza mchezo wa ugenini wa Europa League dhidi ya Rapid Wien mchezo ambao walipata ushindi wa 1-0, kocha wake alithibitisha kuwa hajamuacha mchezaji huyo bali aligoma kusafiri na timu baada ya kuvuliwa unahodha.
Inadaiwa kuwa Mauro Icardi ameshafikia makubaliano ya siri na Juventus na anaweza kajiunga na timu hiyo mwisho wa msimu baada ya hali kuwa mbaya katika uhusiano wake na kocha wake, hiyo ni kwa mujibu wa mwandishi Valer De Maggio wa mtandao wa habari za michezo nchini Italia calciomercato.com unaoaminiwa kwa habari za uhakika.
Hata hivyo sasa chache baada ya taarifa hizo kuwa gumzo mtandao Mauro Icardi akaendelea kuziwekea nguvu tetesi hizo kufuatia post yake ya instagram inayooeleza kuwa “Ni bora kufunga kinywa chako na kuonekana mpumbavu kuliko kuufumbua na kuongea na kuondoa mashaka yote”