Pochettino aweka imani kwa Son
“ Wakati ujao Son akifunga nitaenda katika vyumba vya kubadilishia nguo, nioge na kusubiri mechi iishe “
Hayo ni maneno ya kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino baada ya kuambiwa timu yake imeshinda kila mechi ambayo Son amefunga msimu huu.
Tottenham wameshinda mechi zote 13 msimu huu ambazo mchezaji huyo kutoka Korea Kusini amefunga.
Moja ya mechi hizo ni mechi ya jana ya klabu bingwa Ulaya hatua ya 16 Bora ambapo walicheza na Borussia Dortmund katika uwanja wa Wembley, Son Heung-min akifunga goli la kwanza katika ushindi wa 3-0.