Pigo juu ya pigo kwa PSG kuelekea mechi ya Man United
Timu ya Manchester United sasa imeanza kupewa nafasi kubwa ya kuondoka na matokeo chanya siku ya Jumanne ya Februari 12 wakati wa mchezo wa kwanza wa 16 bora wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa ambayo itakuwa Old Trafford kucheza mchezo huo.
Manchester United wanapewa nafasi hiyo ya kufanya vizuri zaidi kutokana na timu ya PSG sasa kuendelea kukumbwa na pepo la wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kuzidi kupata majeraha, achana na ishu za kumkosa Neymar kwa kuumia mguu na kumkosa Edinson Cavan kwa kuumia mguu pia, PSG sasa imethibitisha rasmi itamkosa beki wake Thomas Meunier.
PSG imethibitisha pia itamkosa nyota huyo Thomas Meunier ambaye aliomba kufanyiwa mabadiliko wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu Ufaransa Ligue 1, hiyo inadaiwa ni baada ya kugongana kichwa na Kamano, hata hivyo mchezo huo dhidi ya Bordeux timu ya PSG ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Edinson Cavani kwa penati, hivyo sasa PSG itacheza dhidi ya Manchester United pasipo uwepo wa Neymar, Cavani na Thomas Meunier.