Hazard akataa kukubaliana na Sarri
Kocha wa Chelsea Maurizo Sarri anatamka nyota wake Eden Hazard afunge magoli mengi zaidi lakini mchezaji huyo amesema hadhani kama ataweza kufanys hivyo.
Hazard tayari amefunga magoli 12 katika ligi kuu nchini England msimu huu , magoli manne nyuma ya magoli aliyofunga katika msimu wake bora akiwa na the blues, msimu wa 2016-17 akifunga magoli 16.
Licha ya kuwa hatari akiwa mbele ya magoli lakini Hazard anadai kuwa matakwa ya Sarri ni makubwa sana.
Hazard ambaye pia ametoa pasi za mabao 10 katika mechi zake 24 za kwanza katika ligi msimu huu akiongea na mtandao wa The Times amesema “ Mimi sio mbinafsi kabisa “
‘ Kwa jini nilivyo inaweza ikawa udhaifu wa kuwa mchezaji bora duniani. Meneja kama Jose Mourinho, Antonio Conte, na sasa Sarri wanataka nifunge magoli 40,50 kwa msimu , lakini ninaweza kufanya hivyo ? Sina uhakika.
‘ Labda wanafikiri ninaweza. Lakini ninajijua mwenyewe na sifikirii ninaweza. Lakini nitajaribu ‘
Eden Hazard,28, katika miaka sita na nusu aliyokaa darajani amewahi kushinda ubingwa wa ligi kuu mara mbili, kombe la ligi, FA Cup pamoja na Europa League.