Maneno ya Mourinho yanaishi Old Trafford
Pamoja na kuwa kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho alifukuzwa kazi katika klabu hiyohivi karibuni kwa tuhuma za mwenendo mbaya wa timuna kutopata matokeo, kauli yake imeendelea kuishikufuatia kusema kuwa Manchester United mwaka mpyaitakuwa TOP 4.
Mourinho alitoka kauli hiyo kufuatia kusuasua kwa timu yake huku hofu ikitanda kuwa kwa mwendo aliyokuwa anaenda nao na timu hiyo, wanaweza wakakosa nafsi yakucheza michuano ya klabu Bingwa Ulaya kama watashindwa kumaliza TOP 4 yaani nafasi nne za juu katika Ligi Kuu ya nchini England
Ushindi wa 3-0 ugenini wa Manchester United dhidi yaFulham umekamilisha maneno ya Jose Mourinho kuwatimu hiyo itaingia TOP mwaka mpya wa 2019 kituambacho Februari 9 2019 imefanikiwa kuingia TOP 4 kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Chelsea walio nafasi ya tano kwa sasa wakiwa na alama 51 naManchester United wakiwa na alama 51 ila Manchester United imewazidi Chelsea mchezo mmoja.
Matumaini ya Manchester United kuwa wamerudi jumlaTOP 4 yanakuja kufuatia Chelsea licha ya kuzidiwa mchezo na Manchester United lakini leo ana mchezomgumu ugenini dhidi ya bingwa mtetezi wa taji hiloManchester City, mchezo ambao utachezwa saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki, Pogba ambaye alikuwa haelewani na Jose Mourinho kabla hajarithiwana kocha wa mpito Ole Gunnar Solskjaer ndio amefunga mabao mawili ya Manchester United kati ya matatu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Fulham.