Beckham kuweka historia mpya Marekani
Nyota wa zamani wa Man United, Real Madrid David Beckham anataraji kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya ligi ya soka nchini Marekani (MLS) kujengewa sanamu yake.
Timu ya LA Galaxy ya MLS ambayo Beckham aliichezea kwa miaka sita tangu ajiunge mwaka 2007, imepanga kumjengea mchezaji huyo sanamu nje ya uwanja wao na kuizindua mwezi ujao.
Timu hiyo imepanga kufanya hivyo ikiwa ni kutoa heshima kwa Muingereza huyo ambaye aliwasaidia kushinda kombe la MLS mwaka 2011 na 2012 na ujio wake katika ligi hiyo uliwavutia mastaa wengine kutoka Ulaya kwenda kucheza, kama vile Thiery Henry, Didier Drogba , David Villa na wengine wengi
Sanamu hiyo itajengwa karibu na mlango mkuu wa kuingia uwanjani na kuzinduliwa katika mechi yao ya kwanza ya msimu Machi 2 wakicheza na Chicago Fire. Beckham anatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo.