Petit ahoji sababu za kufukuzwa Wenger
Moja kati ya vipigo vya mashabiki wa soka la barani Ulaya vilivyokuwa vinazungumzwa sana ni pamoja na kipigo cha Arsenal kilichotokea dhidi ya Manchester City katika uwanja wa Etihad katika jiji la Manchester, Arsenal walifungwa kwa mabao 3-1 na kushushwa hadi nafasi ya 6 na Manchester United kupanda.
Baada ya kipigo hicho kupokea wengi wamezungumza na kuhoji ufanisi na mabadiliko aliyoyaleta kocha mpya wa Arsenal Unai Emery kuwa yanaweza kuwa hayajaishaidia timu na kujikuta ikipokea kipigo chake cha pili katika mechi zake tano za Ligi Kuu nchini England zilizopita wakishinda tatu.
Emmanuel Petit ambaye amecheza Arsenal kati ya mwaka 1997 na 2000 bado hajafurahishwa na muonendo wa Arsenal katika kipindi cha usajili na kuhoji kwa nini Wenger alitimuliwa
“Kama unamfukuza kocha Arsene Wenger na unamwambia kocha (Unai Emery) aliyekuja kurithi kiti chake kuwa huna pesa za kufanya usajili wa wachezaji wapya, ninaweza kuhoji ni nini lilikuwa lengo la kumfukuza kocha Arsene Wenger .” swali la nguli wa Arsenal Emmanuel Petit alipohojiwa na Independent
Kwa sasa kikosi cha Arsenal kilicho chini ya kocha wao Unai Emery aliyemrithi Arsene Wenger aliyekuwa kadumu na timu hiyo kwa miaka 22, wapo nafasi ya sita wakiwa na alama 47 tofauti na alama moja dhidi ya Manchester United walipo nafasi ya tano, Arsenal wamecheza michezo 25, wameshinda michezo 14, droo wametoka michezo mitano na wamepoteza michezo 6 hadi sasa.