Mourinho akwepa kwenda jela
Kocha Jose Mourinho amehukumiwa mwaka mmoja jela nchini Hispania kwa kosa la ukwepaji kodi, lakini hatatumikia kifungo hicho kutokana na sheria za nchi hiyo.
Badala ya kifungo atalipa faini ya pauni 160,000 (Tsh Milioni 483) na faini nyingine ya ziada pauni milioni 1.7 (Tsh Bilioni 5)
Mreno huyo alikwepa kodi ya pauni milioni 2.9 (Tsh Bilioni 8) kati ya mwaka 2011 na 2012 akiwa kocha wa Real Madrid.