Douglas Costa apata ajali
Nyota wa Brazil anayecheza katika klabu ya Juventus ya nchini Italia Douglas Costa amepata ajali akiwa na gari lake binafsi akiwa njiani Kaskazini mwa nchi ya Italia.
Costa amepata ajali hiyo akiwa njiani Kaskazini mwa nchi ya Italia akiwa anarudi Turin ambapo ndipo makao makuu ya klabu yao ya Juventus yalipo baada ya kuwa wamepewa mapumziko ya siku mbili baada ya mchezo dhidi ya Parma, ajali hiyo iliyohusika na magari mengine imetokea akiwa katika gari yake aina ya Jeep Chereokee.
Kwa upande wa mchezaji huyo Douglas Costa amefanikiwa kutoka salama bila majeraha yoyote ila dereva aliyekuwa anaendesha gari la Fiat Punto liligongana na Jeep ya mchezaji huyo, ndio alilazimika kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya gari hiyo kuumia vibaya na yeye kuumia.