Cristiano Ronaldo arudi Ureno
Cristiano Ronaldo akiandamana na mpenzi wake Georgina Rodriguez, jana jumapili alikuwepo kwenye uwanja wa Jose Alvalade nchini Ureno kushuhudia timu yake ya zamani Sporting Lisbon ikicheza dhidi ya wapinzani wao wa jadi Benfica.
Mechi hiyo ambayo inafahamika kwa jina la Derby de Lisboa, ni moja ya mechi kali zaidi nchini Ureno.
Ronaldo alishuhudia timu yake hiyo ikiwa katika uwanja wa nyumbani ikikubali kipigo cha goli 4-2 kutoka kwa mahasimu wao Benfica.