Wanga:Sijioni kama kocha
Mshambulizi wa timu ya Kakamega Homeboyz, Allan Wanga anasema hapanii kuingia katika kazi ya ukufunzi licha ya kuiongoza timu yako kuvuna ushindi Mkubwa didhi ya Bandari siku ya Jumatano.
Wanga aliteuliwa kama kocha mshikilizi siku ya Jumanne baada ya Mganda Paul Nkata kuondoka kwenye timu hiyo.
Mshambulizi huyo wa zamani wa timu ya Azam alifunga mabao mawili kwenye mechi hiyo kabla ya kuondoka uwanjani na kwenda kwenye kiti ya mkufunzi.
Licha ya kushinda mechi hiyo kama Kocha-mchezaji, Wanga anasema hajioni kama kocha kwa sasa.
“Sijioni kama kocha kwa sasa, mimi ni kiongozi tu kwa timu lakini si mkufunzi. Kwa sasa nataka kusaidia timu iandikishe matokeo mazuri tu. Miaka ijayo nitasomea sayansi ya michezo na baada ya hiyo nitaamua kama nitazamia ukufunzi,” alisema Wanga.
Homeboyz ilikuwa imekosa kuandikisha ushindi kwa mechi saba kabla ya kuchapa Bandari.