Sala akumbukwa na Nantes
Klabu ya Nantes jana wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walicheza dhidi ya St.Etienne, ikiwa ni mechi yao ya kwanza tangu mchezaji wao wa zamani Emiliano Sala kupotea na ndege pamoja na rubani wakiwa safarini kutoka France kwenda Cardiff Wales Januari 21 mwaka huu.
Kila mchezaji wa Nantes katika mechi hiyo alivaa jezi iliyoandikwa jina la ‘Sala’ mgongoni mwake
Katika dakika ya 9 ya mechi hiyo mwamuzi Frank Schneider alisimamisha mchezo kwa dakika moja ambapo wachezaji na watu waliokuwepo uwanjani walisimama na kupiga makofi ikiwa ni ishara ya kumkumbuka mchezaji huyo. ( Sala alikuwa anavaa jezi namba 9 akiwa Nantes)
Kocha wa Nantes Vahid Halilhodzic alishindwa kuzuia machozi yasitoke machoni mwake.
Mchezo huo uliisha kwa sare ya 1-1.