MAROUANE FELLAINI ANAFUATA PESA ZA WASTAAFU CHINA
Moja kati ya usemi maarufu kwa mashabiki wawanasoka mahiri barani Ulaya ni pale wanaposikia kuwawachezaji wawapendao wanaondoka Ulaya na kwendakucheza soka Marekani au China, wengi husema kuwawanaenda kuchukua fedha za pensheni kwani huwawanaondoka wakiwa wana umri mkubwa.
Leo imeripotiwa taarifa mpya kuwa kiungo waManchester United raia wa Ubelgiji Marouane Fellainiyupo mbioni kujiunga klabu inayocheza Chinese League, Fellaini ambaye anaonekana kukosa nafasi chiniya kocha wa mpito wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer aliyemchezesha kwa jumla ya dakika 30 katikamichezo miwili ya Crystal Palce na Reading katika yamichezo nane aliyoiongoza Manchester United nakushinda yote.
Jumanne mchana ndio Fellaini karipotiwa kukutana na mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Wood nakuzungumzia hatma yake kuhusu ishu ya kuhama, kamaFellaini atahama atakuwa anahama baada ya kudumu natimu hiyo kwa miaka mitano toka pale alipojiunga nayo2013 akitokea Everton na kuichezea jumla ya michezi177 na 106 akipata nafasi ya kuanza, amefunga mabao22 na pasi za usaidizi wa magoli 6 akicheza kwa jumlaya dakika 10,446 akioneshwa kado 30 za manjano nanyekundu 3.
Fellaini mwenye umri wa miaka 31 atakuwa na takribanimwezi mmoja kuamua hatma yake kama kweliamedhamiria kwenda China au vinginenvyo , kwanidirisha la usajili nchini China litafungwa mwezi Februari28 2019, hivyo hiyo ni nafasi nzuri kwake ya kukaakufikiri na kufanya maamuzi sahihi.