Fabregas ammwagia sifa Thierry Henry
Nyota wa zamani wa timu za Arsenal, Barcelona na Chelsea Cesc Fabregas ameamua kuongea hadharani na kumsifia aliyekuwa kocha wa AS Monaco Thierry kuwa pamoja na kudumu na timu hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu lakini kwake ni kocha anayeweza kuwa juu zaidi.
Cesc Fabregas aliamua kuwa mkweli na kueleza kuwa moja kati ya sababu kuu zilizomfanya yeyem aamue kujiunga na AS Monaco akitokea Chelsea wakati huu wa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari ni kocha Thierry kuwa ndio alimuita, hivyo hiyo ndio sababu kuu ya yeye kuamua kuhama Chelsea na kujiunga na AS Monaco.
Cesc Fabregas na Thierry Henry wakiwa wanacheza wote Arsenal
“Sitadanganya moja kati ya sababu kuu za mimi kuamua kuja kujiunga na AS Monaco ni Thierry Henry aliniita” alisema Cesc Fabregas ambaye amekiri pia chini ya Kocha Leandro Jardim anaamini watafanya kazi vizuri
Nyota huyo ambaye anasimamiwa na wakala mmoja na Thierry Henry alijiunga na AS Monaco Januari 11 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu kwa ada ya uhamisho ambayo ni siri, na amefanikiwa kucheza michezo mitatu tu chini ya Thierry Henry ambaye alifutwa kazi katika timu hiyo baada ya kudumu nae kwa siku 104, Henry alifutwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamrithi Leandro Jardim.