Emiliano Sala kuanza kutafutwa tena
Bado dunia ya soka ipo katika hali ya kuhuzunika kuhusiana na kupotea kwa ndege iliyokuwa imbeba mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Salama pamoja na rubani wake kupotea na kutopatikana hadi leo, sintofahamu imetanda kama watu hao wapo salama au wamekufa kufuatia kutoonekana kwao.
Imefika wiki sasa toka ndege ndogo binafsi aliyokuwa ameipanda Emiliano Sala na rubani wake wakitokea Nantes kuaga wachezaji wenzake wa zamani kuelekea Cardiff kupotea, utafutaji wa ndege hiyo ulifanyika kwa saa 80 bila mafanikio huku tukiambiwa umefanyika wa ardhini na majini kuhakikisha wanapatikana wakiwa hai au wamekufa.
Bahati mbaya baada ya Polisi kuitafuta katika pwani ya Guernsey na kutoonekana, walitangaza rasmi kusitisha zoezi la kuwatafuta watu hao, hivyo wachezaji na watu wa soka mbalimbali waliamua kuchanga pesa ili waendeshe utafutaji binafsi wa kuhakikisha wanapata jibu kuhusiana na Emiliano Sala na rubani wake kama wamepata ajali ni yako wapi mabaki ya ndege na miili yao.
Taarifa iliyotoka ni kuwa baada ya jitihada za kuchangisha pesa kufanikiwa na kupata muitikio mkubwa, zoezi la utafutaji wa ndege hiyo linaanza upya ila inaripotiwa kuwa kwa sasa wataichunguza zaidi chini ya bahari kujua kama ilizama sehemu, taarifa zilizoripotiwa na mamlaka ya ndege Nantes Ufaransa ni kuwa ndege hiyo ilipotea kwenye rada ikiwa katika pwani ya Guernsey
Tukukumbushe tu Jumamosi ya Januari 19 mwaka huu Emiliano Sala alijiunga na Cardiff City akitokea Nantes FC kwa ada ya pauni milioni 15 ila baada ya kusaini alirudi Nantes kuaga wachezaji wenzake na jumatatu jioni kuanza safari ya kurejea Cardiff , hata hivyo akiwa safarini Sala alituma voice note kwa wachezaji wenzake wa Nantes kuwa ana wasiwasi sana na ndege hiyo ikitokea imepita saa moja na nusu hawajasikia chochote kutoka kwake basi watume mtu akamtafute, hadi sasa zaidi ya watu 4000 wamechangia kiasi cha euro 300000 ili kuanza zoezi binafsi la uokoaji.