Meseji za Neymar zatumika kumsajili De Jong Barca
Imeripotiwa kuwa moja kati ya maamuzi ya mshambuliaji wa soka wa timu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar kuwahi kujutia basi ni uamuzi wake wa kuondoka katika timu ya FC Barcelona na kwenda Ufaransa kujiunga na timu ya PSG ambayo inaelezwa Ligi yao ni duni ukilinganisha na Ligi Kuu Hispania (LaLiga)
Inaelezwa kuwa baada ya Neymar kuhama timu hiyo na kwenda Ufaransa aliwahi kutuma ujumbe wa meseji kwa Rais wa Barcelona na kumwambia kuwa anajutia uamuzi wake kwani ameenda kucheza katika Ligi duni ukilinganisha na LaLiga ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.
Kufuatia masononeko hayo ya Neymar kwa Rais wa Barcelona inaelezwa kuwa uongozi wa FC Barcelona wakati wanamfuatilia Frenkie de Jong kutokana Ajax ili ajiunge na timu yao walimuonesha meseji za Neymar akijutia uamuzi huo wa kuhama Barcelona na kujiunga na PSG, hivyo walimuonesha meseji kama sehemu ya kumshawishi asije akadanganyika na pesa na kwenda PSG, kama hufahami Frenkie de Jong aliyesaini na FC Barcelona alikuwa akiwindwa pia na PSG.
Frenkie de Jong mwenye umri wa miaka 21 amesajiliwa na FC Barcelona kutokea timu ya Ajax ya nchini kwao Uholanzi ila atajiunga na Barcelona mwishoni wa msimu wa 2018/2019 hata hivyo Neymar amekuwa akituma meseji kwa viongozi wa Barcelona na kueleza dhamira yake ya kutaka kurudi huku akieleza kuwa havutiwi na hali ya hewa ya Ufaransa.