Ujumbe wa Pogba kwa mchezaji mdogo aliyefia uwanjani
Kiungo wa timu ya Manchester United yenye makaziyake katika jiji la Manchester nchini Uingereza Paul Pogba ameamua kutuma ujumbe wake wa pole na farajakwa kijana na familia ya mtoto wa miaka 15 aliyepoteza maisha uwanjani wakati akicheza soka kwa tatizo la moyo.
Kijana Vitarela mwenye umri wa miaka 15 alipoteza maisha uwanjani kwa ugonjwa wa moyo (heart attack) wakati akiichezea timu yake ya FC Lescar Jumapili iliyopita, kifo hicho kimewagusa watu wengi wa familiaya soka hususani watu wa Ufaransa.
Paul Pogba ambaye ni mshindi pia wa taji la Kombe la dunia alikuwa sehemu ya kikosi cha Manchester United kilipata ushindi juzi wa mabao 3-1 dhidi ya Arsenal mchezo wa FA Cup, ameutoa ushindi huo kwa Vitarela ambaye amewagusa watu wengi wa soka nchni Ufaransa kutokana na nyota yake kuzima akiwa bado mchanga.
Vitarela alikuwa akiitumikia FC Lescar toka akiwa naumri wa miaka 7 hadi U-15 ambayo amuti umemkutaakiwa anaitumikia Hata hivyo Pogba pia aliweka ujumbewa faraja kwa kinda huyo ambaye kifo chake kimelizawatu wengi.
“Nina-hakika kwa sasa unacheza mpira peponi kijana mchanga 🙏🏻, maombi yetu Mungu ataifariji familia yako” aliandika Paul Pogba kuhusiana na msiba huo,
Inaripotiwa kuwa nchini Ufaransa katika michezo ya soka kutakuwa na dakika ya kusimama na kuomboleza kabla ya mchezo kuanza.