Kante kudhamini kutafutwa kwa Sala
Taarifa inayoendelea kuumiza watu wa dunia ya soka kwa sasa ni kuhusiana na mshambuliaji wa kiargentina aliyesajiliwa Cardiffi kutokea Nantes ya nchini Ufaransa Emiliano Sala kupotea akiwa kwenye ndege na rubani wake,imebaki kuhisiwa tu kuwa ndege waliyokuwa Emiliano Sala na rubani wake itakuwa ilipata ajali.
Habari hizo hazijathibitika na kikosi kazi cha uokoaji jana kilitangaza kusitisha zoezi la kuwatafuta watu hao baada ya kuwatafuta kwa muda mrefu pasipo kuona hata dalili la baki la ndege baharini na nchi kavu, kufuatia kusitishwa kwa zoezi hilo sasa baadhi ya wachezaji kama Rabiot na kocha wa Nantes, Gundogun wa Manchester City, Koulibaly wa Napoli na wengine wengi wameripotiwa kuchangisha hela za kulipa kikosi maalum kiendelee na msakako wa kuwatafuta watu hao.
Hata hivyo licha ya wachezaji hao na watu mbalimbali wa familia ya soka kudaiwa hadi sasa kujichangisha kiasi cha pauni 160000 na zaidi kwa ajili ya zoezi hilo, leo imeripotiwa kuwa nyota wa Chelsea Ngolo Kante ameahidi kulipia gharama zote ili akatafutwe Emiliano Sala ambaye wamewahi kucheza pamoja katika klabu ya Caen.
Wawili hao walicheza pamoja mwaka 2015 Emiliano akijiunga kwa mkopo wa muda mfupi akitokea Bordeaux kabla ya kujiunga na Nantes, wakati Kante akiwa ana miaka miwili katika timu hiyo kabla ya kutawanyika huyu akienda Nantes na Yule akienda Leicester City.