Djokovic aweka rekodi mpya Australian Open
Novak Djokovic bingwa Australian Open 2019.
6-3,6-2,6-3 ndio ushindi ameondoka nao katika mchezo wa fainali leo dhidi ya Mhispania Rafa Nadal uliochezwa kwa muda wa saa mbili na dakika nne.
Sasa Novak katika mara 7 zote ambazo amecheza fainali ya Australian Open amechukua ubingwa.
Mserbia huyo ,31,anakuwa mchezaji wa kwanza wa kiume kuchukua ubingwa wa Australian Open mara 7, akiwabwaga Roy Emerson na Roger Federer ambao kila mmoja amechukua mara 6.
Novak ambaye ni mchezaji wa tenesi namba 1 kwa ubora duniani kwa wanaume,anachukua ubingwa wa Grand Slam kwa mara ya 3 mtawalia na Grand Slam yake ya 15 kushinda katika Career yake.