Balotelli atuma salamu Nice
Ijumaa mshambuliaji wa zamani wa timu za Manchester City na AC Milan Mario Balotelli alipata nafasi ya kuichezea timu yake mpya ya Olympique Marseille kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa dhidi ya Lille, Balotelli ambaye amejiunga na Marseille akitokea Nice alicheza mchezo huo.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa Balotelli toka ajiunge na Marseille aliingia dakika ya 74 akitokea benchi na kufanikiwa kuifungia timu yake bao moja katika mchezo waliyopoteza kwa mabao 2-1 katika uwanja wa wao wa nyumbani, goli hilo limetafsiriwa kama ishara ya kuwaonesha Nice kuwa wamefanya makosa kumuacha.
Balotelli ambaye alikuwa na misimu miwili mizuri akiwa na Nice kwa kuifungia jumla ya mabao 33 katika misimu yote ila mahusiano yake mabovu na kocha Patrick Vieira ndio yamepelekea kuachwa kwake kama mchezaji huru, Balotelli ikiwa imepita siku moja toka acheze mchezo wake wa kwanza na kufunga ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika .
“Maadamu unaamini katika wewe siku zote utakuja kuwa bora na imara” aliandika Balotelli kutumia ukurasa wake wa instagram