Naomi Osaka Bingwa wa Australian Open
Naomi Osaka Bingwa wa Australian Open mwaka 2019, anachukua ubingwa huu kwa ushindi wa seti 7-6,5-7,6-4 katika mechi ya fainali dhidi ya mwanadada kutoka Czech Petra Kvitova.
Ushindi huu unafanya Mjapan huyo,21, kuwa mchezaji namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake.
Hii ni mara ya pili anachukua ubingwa wa Grand Slam, vile vile anachukua ubingwa wa Grand Slam kwa mara ya pili mfululizo. Mara ya kwanza ilikuwa ni US Open mwaka jana alipochukua kwa kumfunga Serena Williams fainali.