Mchezaji wa Fulham akamatwa na polisi
Mshambuliaji wa Fulham Aboubakar Kamara raia wa Ufaransa Jumatatu aliitiwa polisi kufuatia kugombana na moja kati ya staff wa timu hiyo wakiwa katika uwanja wa mazoezi wa timu, hivyo kufuatia kilichotokea na staff wa timu hiyo uongozi uliita Polisi kwa ajili ya kutatua tatizo.
Inaelezwa kuwa kabla ya hapo Aboubakar Kamara alikuwa kafungiwa na kocha mkuu wa timu hiyo Claudio Ranieri kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha timu hiyo, hivyo mchezaji huyo inadaiwa alienda mazoezini ili kwenda kujua hatma yake katika timu hiyo ndipo ukatokea ugomvi ulisababisha kuitwa Polisi.
Kocha Claudio Ranieri alifikia uamuzi wa kumsimamisha mchezaji huyo kutokana na kubaini kuwa ni kiongozi wa kusababisha usumbufu katika timu, msemaji wa Polisi alithibitisha taarifa za ugomvi huo kwa waandishi wa habari na kueleza taarifa walipozipata.
.
“Polisi waliitwa katika uwanja wa mazoezi New Malden Jumatatu ya saa 17 jioni kwa uharaka baada ya ugomvi kutokea, maofisa wa Polisi walifika na mtu mmoja mwenye umri wa miaka 20 na kitu alikamatwa kwa tuhuma za jinai na alichukuliwa hadi kituo cha polisi London Kusini na hatimaye kuachiwa kwa dhamana uchunguzi ukiendelea”