TOttenham wapata pigo tena
Klabu ya Tottenham Hotspur ya nchini England imetangaza kupokea taarifa ambazo ni pigo katika kikosi chake kufuatia taarifa za kuumia kwa nyota wao wa kiingereza Dele Ali, Spurs wametangaza kuwa nyota huyo ni majeruhi kwa sasa na atalazimika kuwa nje ya uwanja kuuguza jeraha lake.
Dele Ali aliumia nyama za paja weekend iliyopita wakati wa mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliyomalizika kwa Tottenham kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham wakiwa ugenini, kufuatia jeraha hilo na jopo la madaktari wa Tottenham kumchunguza nyota huyo, wametangaza atakuwa nje ya uwanja hadi mwanzoni mwa mwezi wa tatu.
Taarifa hizo zinakuja wakati mbaya zaidi ambapo Tottenham inatoa taarifa hizo ikiwa ni wiki chache zimepita toka nahodha wao Harry Kane aripotiwe kuumia kifundo cha mguu kilichopelekea Tottenham Hotspurs kumkosa katika michezo yake zaidi ya saba ijayo, Spurs sasa ina majeruhi kadhaa wakiwemo mkenya Victor Wanyama, Harry Kane na Dele Ali.