Barca lanasa kinda la Ajax
Klabu ya Barcelona imemsajili kiungo Frenkie de Jong kutoka Ajax kwa ada ya awali ya euro milioni 75 huku akisaini kandarasi ya miaka mitano. Kiungo huyo Mholanzi mwenye umri wa miaka 21, atajiunga rasmi na mabingwa hao wa Hispania Julai 1,2019