Ronaldo apigwa faini nchini Hispania kwa kukwepa kodi
Staa wa Juventus Cristiano Ronaldo amekubali kulipa faini ya pauni milioni 17 (Tsh Bilioni 50) na kifungo cha miezi 23 jela kwa kosa lake la kukwepa kodi kati ya mwaka 2011 na 2014 nchini Hispania wakati anaichezea Real Madrid.
Hata hivyo hatatumikia kifungo hicho kufuatia kuwa nchini Hispania hawatumikii kifungo cha chini ya miaka miwili kwa mtuhumiwa wa mara ya kwanza.
Kodi hiyo ya pauni milioni 13 (Tsh Bilioni 38) ambayo aliikwepa ni inahusiana na mapato yake ya nje ya uwanja na haki za picha zake.
Imeelezwa kuwa Ronaldo alimuomba jaji ahudhurie kesi hiyo leo kwa kutumia kanda ya video lakini akakataliwa, baada ya kukataliwa akaomba aingie na gari mahakamani ili akwepe vyombo vya habari lakini pia akakataliwa.