Mchezaji wa Cardiff apotea na ndege
Mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala alikuwa kwenye ndege binafsi iliyopotea angani jana ikiwa inatoka Nantes,France kwenda Cardiff Wales, wamethibitisha mamlaka ya anga ya France.
Muargentina huyo,28, aliyesajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 15, alikuwa ni miongoni mwa watu wawili waliokuwepo kwenye ndege hiyo iliyopotea.
Baada ya kusaini mkataba siku ya jumamosi, Sala alirejea nchini France kuwaaga wachezaji wa timu yake ya zamani ya Nantes, na baadae kuweka picha akiwa na wachezaji hao katika Instagram akiandika “ Kwa heri ya mwisho “ kabla ya kupanda ndege kurejea Wales.
Afisa anayehusika katika kuitafuta ndege hiyo John Fitzgerald anasema kuwa hatarajii kumkuta mtu yoyote akiwa hai
.
“ Kuna bahati ya asilimia 5 tu ya kuwapata Sala na rubani “ alisema Fitzgerald. ‘ Maji ni ya baridi sana kwa sasa , kwa hiyo kama kuna ambaye amepona kwenye maji , ni baridi sana , ni saa moja tu unaweza kuwa mzima katika kipindi hiki cha mwaka ‘
.
Familia ya mchezaji huyo ipo nchini Argentina na baba wa mchezaji huyo Horacio amesema alijisikia vibaya sana baada ya kupata taarifa za kupotea kwa mwanae.