Hector Bellerin nje msimu mzima
Beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin anataraji kukaa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu uliobaki kufuatia kuumia goti lake la kushoto katika mechi dhidi ya Chelsea jumamosi iliyopita
Imeripotiwa kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita mpaka tisa.
Mechi hiyo ya Chelsea ndio ilikuwa mechi yake ya kwanza kurejea uwanja tangu aumie katika shavu la mguu mwezi Disemba kwenye mchezo dhidi ya Southampton.
Hili ni pigo kwa kocha Unai Emery ambaye sasa itampasa kuwatumia Ainsley Maitland-Niles, Stephan Lichtsteiner na Carl Jenkinson kuziba pengo.