HII NDIO ORODHA YA WACHEZAJI WA SIMBA WALIOENDA CONGO
Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC jana asubuhi imesafiri kuelekea Kinshasa Congo kwa ajili ya mchezo wake wa pili wa michuano ya klabu Bingwa Afrika hatua ya Makundi dhidi ya AS Vita, Simba anaenda Congo akiwa kinara wa Kundi D akiwa ana alama tatu sawa na Al Ahly ila anakuwa kinara kwa tofauti ya bao moja.
Hata hivyo Simba SC ukiachana na kuwa tayari inamkosa beki wake Shomari Kapombe kwa muda mrefu, Erasto Nyoni aliyeumia Mapinduzi Cup 2019, inaenda kucheza na Congo ikiwa na pigo la kumkosa nahodha wake John Bocco huku AS Vita pia itamkosa mlinzi wake Dharles Mondi anayetumia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonesha dhidi ya Al Ahly.
Simba wameenda na kikosi cha wachezaji 19 kupambana na AS Vita ambao tayari hawana alama hata moja kufuatia kipigo cha bao 2-0 waliyofungwa katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Al Ahly nchini Misri, hiki ndio kikosi kamili cha SImba kilichoenda Congo Aishi Manula, Deogratus Munish, Nikolaos Gyan, Paul Bukaba, Pascal Wawa, Juuko Murshid, James Kotei, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Clatous Chama, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi, MO Ibrahim, Adam Salamba, Rashid Juma, Shiza Kichuya, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Mzamiru Yassin.