Fellaini nje mwezi mmoja
Kiungo wa Man United Marouane Fellaini atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu au nne baada ya kuumia kwenye shavu la mguu akiwa mazoezini, amethibtisha kocha wa muda wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer
Kocha huyo pia amesema Alexis Sanchez yupo fiti kucheza mechi ya kesho dhidi ya Brighton baada ya wiki jana kuukosa mchezo dhidi ya Tottenham.