RICARDO KAKA AMETAJA MCHEZAJI WAKE BORA KUWAHI KUCHEZA NAE KATIKA MAISHA YAKE YA SOKA
Mchezaji wa zamani wa timu za Real Madrid, AC Milan na timu ya taifa ya Brazil Ricardo Kaka ni moja kati ya viungo bora kuwahi kutokea katika soka, pamoja na umahiri wake wa kucheza uwanjani na kufanya vitu muhimu katika mchezo, sasa leo Kaka ametaja wachezaji wake bora aliowahi kucheza nao uwanjani.
Kaka ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kusimama na kuwashinda Messi na Ronaldo katika tuzo ya Ballond d’Or 2007, ametaja orodha ya wachezaji wake anaowakubali lakini mbrazil mwenzake Ronaldo De Lima ana mkubali zaidi kutokana alikuwa akifanya vitu vya kumshangaza uwanjani, Kaka alikuwa anatamani pia angepata bahati ya kucheza na Zidane.
“Mchezaji bora niliyewahi kucheza nae ni Ronaldo, nachagua mchezaji kutokana na uwezo wake wa kufikiri na kutekeleza majukumu yake uwanjani, Cristiano na Ronaldinho ni wachezaji bora lakini nilimuona Ronaldo anafanya vitu ambavyo vinanifanya niwaze vimewezekana vipi kufanyika, natamani pia ningecheza na Zidane pia” alisema Ricardo Kaka katika mahojiano maalum
Tukukumbushe Ricardo Kaka ambaye amezaliwa April 22 1982 Gama Brazil katika familia ya baba injinia na mama mwalimu, amewahi kucheza vilabu mbalimbali katika maisha yake ya soka ikiwemo Sao Paulo ya nchini kwao Brazil, AC Milan ya nchini Italia kwa nyakati mbili tofauti, Real Madrid na Orlando City.