GARY NEVILLE AMEBADILI AMEWAONYA WALIMU WASIBADILI FALSAFA YA MANCHESTER UNITED
Mkongwe wa timu ya Manchester United aliyewahi kucheza katika timu hiyo kwa miaka 19 Gary Neville akihojiwa na Sky Sports ameeleza kuhusiana na walimu wanaokuja Manchester United kuheshimu falsafa ya Manchester waliyoikuta na wasibadilishe.
Neville ameweka wazi mtazamo wake ikiwa ni miezi michache imepita baada ya kufukuzwa kwa kocha Jose Mourinho, ambaye inaelezwa kuwa alifeli katika timu hiyo kutokana na kutaka kuanzisha falsafa yake mpya katika soka ya kucheza mpira wa kujihami zaidi, hivyo anashauri makocha wasijaribu kubadili falsafa na asili ya soka safi la kushambulia na kuburudisha.
“Hakuna atakayeruhusiwa kuingia katika uwanja wa mazoezi wa Manchester United au Old Trafford kuanzisha falsafa mpya, hilo limeisha Manchester United falsafa ina maana kubwa kama ilivyo kwa timu za Barcelona au Ajax, soka la Manchester United linachezwa kwa haraka, linachezwa soka la kushambulia katika njia ya kuburudisha unawaleta wachezaji wachanga unawaamini unawapa nafasi na mnashinda” alisema Neville
Tukukumbushe tu Gary Neville mwenye umri wa miaka 43 aliwahi kuichezea Manchester United kwa muda wote wa maisha yake ya soka kuanzia timu za vijana za timu hilo (1991-1992) na timu ya wakubwa kuanzia 1992-2011 na kwa sasa amepewa shahada ya heshima ya udaktari kutoka chuo Kikuu cha Salford mwaka 2014.
