ZAHERA KATOLEA UFAFANUZI SUALA LA TUHUMA ZA MAKAMBO KUTOWEKA
Mwalimu wa klabu ya Yanga raia wa Congo na Ufaransa Mwinyi Zahera jana aliamua kumaliza uvumi kuhusiana na madai ya mchezaji wake raia wa Congo DR Herieter Makambo kama ni kweli ametoroka kambini na kwenda kusikojulikana bila ya ruhusa maalum au kuna taarifa nyingine.
Zahera ameeleza baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya Mwadui FC uliyomalizika kwa Yanga kupata alama tatu kwa kuifunga Mwadui FC ya mkoani Shinyanga kwa mabao 3-1, ameeleza kuwa taarifa za kupotea kwa Makambo na kudaiwa kazima simu ni uongo.
Ukweli ni kuwa mchezaji huyo yupo kwao Congo kwa ruhusa maalum na wanaosema amezima simu waongo, kwani Tanzania hii wenye namba za Makambo za Congo ni yeye na mlinda mlango wake Klaus Kindoki anayetoka taifa moja na Makambo nchini Congo.
“Tunatoka Mbeya kwa ndege Makambo anaenda nyumbani kwake, wanasema Makambo alikuwa kambini wapi usiku saa nane Makambo anashika ndege anaenda Congo, kazima simu wapi wewe una namba ya Makambo ya Congo? Tulio na namba ya Makambo ya Congo ni mimi na Kindoki” alisema Mwinyi Zahera mbele ya waandishi wa habari baada ya kuiwezesha Yanga kuendelea kuongoza Ligi kwa kuwa na alama 53 wakikamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi msimu wa 2018/19.