Paul Pogba aripotiwa kupata mtoto
Kiungo wa Man United Paul Pogba na mpenzi wake, Maria Salaus jana usiku walionekana wakielekea katika mgahawa mmoja unaoitwa The Ivy Restaurant huko jijini Manchester na kuzuka tetesi za mchezaji huyo tayari amekuwa baba kufuatia tumbo la ujauzito alilokuwa nalo mpenziwe kutoonekana.
Mwanadada huyo raia wa Bolivia alionekana na tumbo la ujauzito kipindi cha Christmas mwaka jana wakati akienda katika uwanja wa Old Trafford kushuhudia mechi za Man United.
Pogba licha ya kuwa ni moja ya wachezaji wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii bado hajasema kitu chochote kuhusu kuzaliwa kwa mtoto wake.
Habari za kuzaliwa kwa mtoto wa Pogba awali zilielezwa na gwiji wa Man United Bryan Robson ambaye alisema “ Nilipomuona Paul wiki iliyopita Dubai akiwa na kikosi cha Man United, tulikuwa na mazungumzo mafupi na kumpa hongera kwa kuzaliwa kwa mwanae”
Maneno ya Robson yameonekana na ukweli baada ya mpenzi wa mchezaji huyo kuonekana akiwa hana tumbo lake la ujazito.