“Pogba alistahili kadi nyekundu “- Souness
Mkongwe wa zamani wa timu za Tottenham na Liverpool Graeme Souness amekuwa mkali na kutoa kauli nzito kuhusiana na mwamuzi wa mchezo wa Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspur uliyochezwa jana na kumalizika kwa Manchester United kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Marcus Rashford dakika ya 44 ya mchezo.
Graeme Souness amekasirishwa na uchezeshwaji wa mchezo huo na mwamuzi Mike Dean kwa kusema kuwa mwamuzi huyo hajui mpira alipaswa kumpa kadi nyekundu kiungo wa Manchester United Paul Pogba kutokana na faulo aliyoiita mbaya kumchezea mchezaji wa wa Tottenham Dele Alli.
Mkongwe huyo anaamini kuwa kwa namna Pogba alivyomchezea Dele Alli dakika ya 78 ya mchezo huo alistahili kuoneshwa kadi nyekundu na sio njano kama alivyofanya Mike Dean, tukukumbushe tu Souness aliwahi kuichezea Tottenham mwaka 1970-1972 na Liverpool mwaka 1978 -1984 Liverpool
“Ninafikiri ilikuwa ni kadi nyekundu hakuna chembe hata ya mashaka kuhusiana na hilo katika akili yangu , (Pogba) alikuwa anajua kabisa anafanya nini unamkanyaga na kutumia uimara wako kumtoa mchezaji lakini angalia mpira ulipokuwa na angalia mguu wake ulipokuwa, kama mwamuzi hakuona hiyo kama ni kadi nyekundu ila ameona ilikuwa faulo na ameona alistahili (Pogba) kuoneshwa kadi ya njano basi hajui kitu kuhusu mchezo wa mpira wa miguu” alisema Graeme Souness