Huddersfield waachana na kocha wao
Kocha David Wagner ameondoka katika klabu ya Huddersfield Town baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano. Huddersfield wameshinda mechi mbili tu kati ya 22 walizocheza katika Premier League msimu huu , wakishika nafasi ya mwisho katika ligi hiyo wakiwa na pointi 11.