MATOKEO YA AL AHLY YAMEMPA KIBALI SIMBA CHA KUONGOZA KUNDI D
Baada ya wekundu wa Msimbazi Simba watoto waKariakoo kufanikiwa kupata matokeo chanya katikamchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi wa KlabuBingwa Afrika dhidi ya Js Saoura ya nchini Algeria mabingwa wa kihistoria walio Kundi moja na Simba wanaojulikana kwa jina la Al Ahly wao walicheza usiku wake na kuwaadhibu wacongo klabu yaAS Vita kwa jumla ya mabao 2-0, mabao ya Al Ahlyyakifungwa na Masser Maher dakika ya 65 na Maalouldakika ya 79 kwa adhabu ya mkwaju wa penati. Simba sasa anaongoza Kundi lao D lililokuwa na timu zaJS Saoura, AS Vita na Al Ahly kwa kuwa na alama 3 sawa na Al Ahly lakini Simba anaongoza kwa tofauti yamabao ya kufunga akiwa na mabao 3, wakati Al Ahlymabao mawili. AS Vita ya Congo inaangukia nafasi ya tatu kwa kuwawamefungwa mabao machache (2) dhidi ya Al Ahlykatika kipigo cha mabao (2-0) ukilinganisha na JS Saoura waliyopoteza mchezo kwa kufungwa mabao 3-0, mechi ya pili Simba atacheza ugenini Januari 19 dhidiya AS Vita nchini Congo na JS Saoura atakuwamwenyeji wa Al Ahly Januari 18.