Simba amuua mwarabu Taifa
Goli 3-0 ndio ushindi ambao Simba SC imeanza nao katika mechi yao ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi msimu huu.
Simba SC wameondoka na ushindi huo leo katika dimba la uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya timu ya JS Saoura kutoka nchini Algeria.
Magoli ya Simba leo yamewekwa kimiani na Emmanuel Okwi dakika ya 45 huku mawili mengine yakifungwa na Meddie Kagere dakika ya 52 na 68.
Baada ya kumaliza kibarua cha leo Simba watashuka tena dimbani tarehe 19 Januari kucheza na AS Vita huko nchini Congo.