Pochettino ampa sifa Ferguson
Kuelekea mechi ya Manchester United dhidi ya Spurs siku ya jumapili na siku chache baada ya Ole Gunnar Solskjaer kumsifia kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino kocha huyo wa Tottenham nae sasa ameibuka na kumwaga sifa zake kwa maamuzi ya kocha huyo wa muda wa klabu ya Manchester United ya kumualika aliyekuwa kocha mkongwe wa timu hiyo Sir. Alex Ferguson.
Solskjaer amemualika Fergie katika mazoezi kuongea na wachezaji na pia kuleta bahati Old Trafford.
Pochettino alipoulizwa kama alimtumia salamu za pole Fergie kipindi anaumwa, alisema ndio alituma na kuwa asingeweza ficha hisia zake kwa kocha huyo bora kwa sababu ni moja ya watu waliompa msukumo.
Alisema mambo sasa yamebadilika na klabu yake ya Tottenham sasa imeimarika kuanzia kushindana na timu kubwa kimpira na nje ya mpira.
Tottenham wameshinda mechi zao 3 za mwisho walizocheza na Man United nyumbani katika ligi kuu nchini England.