Ayany, Akwana wasimamishwa kazi
Klabu ya KCB imewasimamisha kazi makocha wasaidizi Ezekiel Akwana na Elvis Ayany baada ya Matokeo mabaya inayoyapata timu hiyo.
Licha ya kuwasajili wachezaji wa haiba kubwa baada ya kupanda daraja mwaka uliopita, KCB haijaweza kupata ushindi katika mechi tano ya kwanza msimu huu, timu hiyo imeweza kujivunia pointi moja baada ya sare dhidi ya Bandari majuma mawili yaliyopita.
Uongozi wa klabu hiyo umeamua kuwasimamisha kazi kwa muda Ayany na Akwana kwa madai ya kuleta kutoelewana kwenye benchi la ufundi. Kocha mkuu Frank Ouna ataiongoza timu licha ya tetesi kuwa huenda atatimuliwa kazini matokeo ya timu yasipobadilika.
Nahodha wa timu hiyo Dennis Orenge pia ametimuliwa kwenye timu kwa muda kwa madai ya kuwachochea wachezaji wa zamani dhidi ya wale waliosajiliwa hivi majuzi.
KCB itafaana na Kariobangi Sharks siku ya Jumapili katika mechi itakayo andaliwa uga wa Kenyatta mjini Machakos.