Zahera amtumbua Yondani
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameamua kufanya maamuzi magumu ya kumuondoa aliyekuwa nahodha wa timu hiyo Kelvini Yondani katika nafasi hiyo na kuamua kumtangaza nahodha mpya.
Kufuatia maamuzi hayo ya kocha Mwinyi Zahera Yanga sasa nahodha wao mpya atakuwa ni Ibrahim Ajib.
Sababu za kocha Mwinyi Zahera kumuondoa Kelvin Yondani katika nafasi hiyo ni kutokana na beki huyo kuwa na makosa ya kugoma lakini pia amechelewa mazoezini kwa siku moja pasipo kutoa taarifa yoyote.
Inaelezwa kuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alitoa mapumziko ya siku tano kwa wachezaji wake na baada ya hapo walipaswa kwenda mazoezini kama kawaida, hivyo Yondani baada ya siku tano kuisha akaongeza moja pasipo kuomba ruhusa wala kutoa taarifa yoyote kwa kiongozi yoyote.