PEP GUARDIOLA AMESEMA LIVERPOOL WANA PRESHA YA MIAKA 29
Kocha wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza Pep Guardiol ambaye yupo katika mbio za kutetea taji hilo linaloonekana Liverpool amedhamiria kumaliza ukame, Guardiola ameeleza kuwa Liverpool kwa sasa wapo na presha.
Kwa sasa Liverpool ndio anaongoza Ligi Kuu ya nchini Uingereza akiwa na alama jumla ya 54 katika michezo 20 akifuatiwa na Tottenham ambaye tayari amewazidi mchezo mmoja mmoja wote Liverpool na Manchester City lakini Manchester City wako nyuma kwa alama 7 dhidi ya Bingwa wa Mapinduzi.
“Baada ya miaka 29 bila kutwaa taji la Ligi Kuu ya nchini Uingereza hivyo wapo pale kutwaa taji hilo, kwangu hiyo ni hamasa kubwa ya kupambana kuwafikia, kwa nini tusipambane na kuwafikia? Ili tuwape presha zaidi”alisema Kocha wa Manchester City kuelekea mchezo dhidi ya Liverpool
Kwa miaka 29 sasa klabu ya Liverpool haijawahi kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza, hivyo kuwa kwake kinara kuwanawapa nafasi ya kuongeza Ligi na hamasa ya kufanya vizuri zaidi, kutokana na kutotwaa taji hilo kwa miaka mingi hviyo lazima wawe na presha, Guardiola anasema ili kuwaondoa na kuwafunga wakati huu wakiwa na presha