MANCHESTER UNITED YA OLE GUNNAR SOLSKJAER HAUSHIKIKI
Malaika wa Baraka wanaendelea kuishushia kheri klabu ya Manchester United toka kuondoka kwa aliyekuwa kocha wao mreno Jose Mourinho, Manchester United toka aondoke Mourinho na wapewe kocha wa mpito wamekuwa wakipata matokeo.
Kikosi cha Manchester United kikiwa ugenini katika dimba la Newcastle wameendeleza wimbi la ushindi chini ya kocha wao wa muda Ole Gunnar Solskjaer ambaye hadi sasa ameiongoza Manchester United katika michezo minne na kushinda yote na timu yake ikifunga jumla yam abo 14.
Manchester United licha ya kuwa ugenini wameshinda jumla ya mabao 2-0, mabao ya Manchester United yakiwekwa kambani na Romelu Lukaku dakika ya 64 na Marcus Rasford dakika ya 80, Solskjaer kwa sasa anapambania timu yake imalize TOP 4 ili kupata tiketi ya ucheza michuano ya klabu Bingwa Ulaya.
Hata hivyo ushindi huo bado unaifanya Manchester United kuendelea kuwa nafasi ya 6 licha ya kufikisha jumla ya alama 38 wakizidiwa alama 3 na Arsenal waliopo nafasi ya tano na wamezidiwa na alama 6 wakiwa nafasi ya nne.