KOMPANY ANA AAMINI GUARDIOLA HAWEZA KUCHEZA KAMALI NA KUMPANGA KEVIN DE BRUYNE
Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany bado anaamini kuwa kocha wake Pep Guardiola hatokubali kucheza kamari ya kumchezesha Kevid De Bruyne katika mchezo wa leo usiku wa Manchester City watakapoikaribisha Liverpool katika uwanja wao wa Etihad.
Kevin De Bruyne aliikosa safari ya Manchester City siku ya Jumapili kwenda kuwavaa Southampton kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia 100 kutokana ndio kwanza amerejea kutoka kuuguza jeraha lake la pili la goti msimu huu, hivyo Kompany anaamini kuwa ni hatari kucheza kwa De Bruyne akiwa hayupo fiti asilimia 100 sasa anaweza kuumia zaidi.
Kwa upande wa Pep Guardiola yeye alitoa kauli ambayo inaashiria bado ni asilimia 50 kwa 50 kwani hana uhakika kama De Bruyne atamchezesha, mashabiki wa Manchester City wengi wanatamani kuona kuona De Bruyne akirudi dimbani usiku wa leo kutoka na umuhimu wake na ukubwa wa mchezo ina ni hatari kwa jeraha lake anaweza kupata matatizo zaidi.
“Wote tunajua uimara wa Kevin De Bruyne na uwezo wake katika kubadili mchezo uwanjani ila sijui kwa kiasi gani yupo fiti, anaonekana kama yupo timamu lakini nafikiri msimu huu ana vitu vingi sana vya kufanya kwa timu lakini kama nitapewa nafasi ya kuamua ningemuacha awe fiti kabisa kwa ajili ya michezo mingine ya msimu” alisema Vincent Kompany