Solskjaer kuweka kambi Dubai
Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anataraji kusafiri na kikosi chake kuelekea mjini Dubai jumamosi jioni baada ya mechi yao FA Cup dhidi ya Reading
Timu hiyo wanataraji kufikia katika hoteli ya nyota tano ambapo watakaa kwa muda wa siku nne katika mji huo wenye hali ya hewa ya joto.

Kocha huyo anataka kuitumia safari hiyo kuwaweka pamoja wachezaji wake kuelekea mchezo wao dhidi ya Tottenham utakaopigwa Wembley Januari 13.
