Pulisic atua rasmi Chelsea
Klabu ya Chelsea imekamilisha kumsajili winga Christian Pulisic kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya pauni milioni 58.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani,20, atabakia kwa mkopo Dortmund mpaka mwisho wa msimu huu.
Pulisic ambaye ameanza kuitumikia Borussia Dortmund tangu 2016 , anatajwa kuwa moja ya vipaji bora kuwahi kutokea nchini Marekani.