MWINYI ZAHERA ATAJA TIMU ZINAZOWEZA KUIZUIA YANGA KUTWAA UBINGWA
Kocha mkuu wa Yanga raia wa Congo na Ufaransa Mwinyi Zahera anaamini timu yake ina uwezo mkubwa msimu huu wa kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania bara lakini akaeleza kuwa ni timu mbili pekee ndio kimahesabu zina uwezo wa kuizuia Yanga kutwaa Ubingwa.
Mwinyi Zahera kati ya timu 19 zinazoshiriki Ligi Kuu msimu wa 2018/2019 ni timu mbili tu kwa mujibu wa hesabu zake ndio zina uwezo wa kuizuia Yanga isitwae taji la Ligi, timu alizozitaja Zahera ni Simba SC ambayo ikishinda viporo vyake vyote itakuwa tofauti ya alama tano na Yanga na Azam FC ambao wao watakuwa na tofauti ya alama 7 dhidi ya Yanga.
“Wanne na watano wameshakuwa na tofauti na sisi na alama karibu 17 au 15, 17 sawa na mechi tano ambazo inafaa wao washinde mechi karibu zote na sisi tupoteze mara tano ndio Yule aliye nafasi ya nne, watano na sita ndio watakuwa na nafasi ya kutuzuiwa kutwaa Ubingwa, mwenye uwezo wa kutuzuia Ubingwa ni Simba ambao wana tofauti ya alama tano wakishinda michezo yao yote na Azam ana tofauti ya alama 7, wale wengine wanaweza kutufunga katika mechi lakini sio kutuzibia Ubingwa”alisema Mwinyi Zahera kupitia Azam TV
Hadi sasa Yanga inaongoza Ligi Kuu ya Tanzania bara ikiwa na jumla ya alama 50, ikifuatiwa na Azam FC waliopo nafasi ya pili wakiwa na alama 40 na kiporo cha mchezo mmoja, Simba wao wapo nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya alama 33 na viporo vya michezo minne ya Ligi Kuu, hivyo wanamtihani wa kuhakikisha wapata matokeo chanya katika viporo vyao ili wawe kutetea Ubingwa wao.