Dullah Mbabe ampiga KO Cheka
Baada ya vuta ni kuvute na kuharibika kwa pambano katiya wanamasumbwi Dullah Mbabe na Francis Cheka kwamadai ya Cheka kukwepa kucheza pambano dhidi yaDullah Mbabe kwa kumuhofia, hatimae Dullah Mbabena Francis Cheka wapanda ulingoni. Jumatano ya Desemba 26 2018 siku ya Boxing Day katika uwanja wa PTA Sabasaba wawili hao walikubalikushuka ulingoni kucheza pambano lao na kumalizaUbishi nani kati yao ni mfalme wa mchezo wa ngumiTanzania ikiwa siku moja imepita toka wapime uzito. Pambano hilo lilifanikiwa kuchezwa na Dullah Mbabekumvua ufalme wa mchezo wa ngumi Bondia Francis Cheka uzito wa kati (Middleweight ) kwa kumpiga kwa Knock Out (KO) round ya sita na kumfanya bondiaDullah Mbabe kutangazwa Bingwa mpya wa WBF, kwamuda mrefu pambano la Cheka na Dullah Mbabelilikuwa likisubiriwa.