SIMBA SC KAZI WANAYO SOBHI KATANGAZA KUTOKA EPL KURUDI KUISAIDIA AL AHLY
Klabu ya Al Ahly ya Misri inaonekana safari hii imedhamiria kweli kufanya kweli katika michuano ya klabu Bingwa Afrika hatua ya makundi inayoanza January 11 2019, Al Ahly imepangwa Kundi D lenye timu za AS Vita Club ya nchini Congo, Simba SC ya Tanzania na JS Saouro.
Kufuatia michuano hiyo hatua ya makundi kuanza Al Ahly imeripotiwa kumrejesha mchezaji wake wa zamani Ramadan Sobhi kutoka klabu ya Huddsfield ya Uingereza kuja kuongeza nguvu katika michuano ya klabu Bingwa ya Afrika, Sobhi atakuwa Al Ahly kwa mkopo wa miezi sita tu.
Sobhi ambaye alikuwa Stoke City kabla ya kwenda Huddsfield zote za nchini Uingereza amethibtisha kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa anarejea Misri kwa ajili ya kuisaidia timu yake ya zamani ya Al Ahly katika michuano ya klabu Bingwa Afrika.
Tukujulishe kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo Simba SC itacheza dhidi ya Al Ahly mwezi Feburary 1 2019 nchini Misri, huo utakuwa ni mchezo wake wa tatu baada ya kucheza dhidi ya JS Saouro nyumbani Dar es Salaa na AS Vita Club nchini Congo.