POGBA AMSAIDIA OLE GUNNAR SOLSKJAER KUWEKA HISTORIA LIGI KUU YA NCHINI UINGEREZA
Kocha wa mpito wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ambaye amechukua nafasi ya Jose Mourinho hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua ni yupi kocha wa kudumua wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer ameanza vizuri na kuweka rekodi, kwa sasa jina la kocha huyo limekaa katika vinywa vya mashabiki wa Manchester United kutokana na kuwarejeshea furaha.
Kwa hivi karibuni kabla ya Jose Mourinho kuondolewa, Manchester United ilikuwa inadaiwa kuwa timu hiyo sasa huwezi kuipa dhama kuwa itapata matokeo chanya hata ikitokea ikacheza na underdog, ila sasa hivi ni tofauti chini ya Ole Gunnar Solskjaer akiiongoza katika mechi tatu.
Manchester United ikicheza dhidi ya AFC Bournemouth Desemba 31 imefanikiwa kupata ushindi wa tatu mfululizo chini ya Ole Gunnar Solskjaer kwa kuifunga Bournemouth kwa mabao 4-1, maboa ya Manchester United yakifungwa na Paul Pogba aliyefunga mawili dakika ya 5 na 33, Marcus Rashford dakika ya 45 na Romelu Lukaku dakika ya 72 wakati bao la Bournemouth likifungwa na Ake dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko.
Ushindi huo unakuwa ni ushindi wa tatu wa mfuluzo wa Manchester United ambao umemfanya Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu Uingereza katika mechi tatu za kwanza kuanza kazi kikosi chake kufunga zaidi ya magoli 10, Paul Pogba nae akifunga manne kati ya hayo na kutoa pasi za usaidizi lakini ushindi huo umewafanya Manchester United kufikisha jumla ya alama 35 lakini bado wanaendelea kusalia nafasi ya 6.